Ijumaa, 30 Novemba 2018

AFC: Alikiba atangaza kumleta Yvonne Chaka Chaka katika Tamasha lake

By

Mkali wa Bongo Fleva Alikiba amedokeza kumleta nchini Mwimbaji mkongwe Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ambapo watatumbuiza pamoja katika Tamasha la‘Funga Mwaka na King Kiba’ litakalofanyika December 22,2018.
Image result for images of alikiba with ivine chakachaka
July mwaka huu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alikiba kumleta nguli huyo nchini  na kufanya mradi wa kuwasaidia wanawake kufanikisha sector mbalimbali katika Bara la Afrika na wawili hao walifanya wimbo wa ‘Akilia Mama’ kwaajili ya mradi huo.
“Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka   huukatika#FungaMwakaNaKingKibazinakuja na show mbili kubwa ndani ya December 2018″
“1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es salaam 22 .December. 2018 

2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018.”

Ijumaa, 9 Novemba 2018

AFC: Tekno avunja ukimya, asema anahitaji kuombewa

By
Image result for images of tekno miles
Msanii Tekno kutokea nchini Nigeria amewaomba mashabiki zake wamuombee hii ni kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu pamoja na kutoonekana kwenye shows.
Tekno ametoa sababu zilizomfanya kuwa kimya kwa muda mrefu kuwa yupo katika hali ya kurudisha afya yake iwe imara ili aweze kurudi katika kazi anayoipenda zaidi ambayo ni muziki na kusisitiza kuwa anahitaji kuombewa ili apone haraka.
“Nimekuwa mbali na pia nikipata matibabu, tafadhali nawaomba msihuzunike nikishindwa kuonekana kwenye shows nilizokuwa natarajiwa kufanya show. Nachukua muda kurejea kwenye hali yangu ya kawaida na ninamatumaini nitarudi kwenye kile ninachokipenda”
“Ninaomba radhi na kama itawezekana kuniombea fanyeni hivyo, Mungu aendelee kutuangalia wote Asante”

 

Source: millard.com :http://millardayo.com/uikmn4ersw2q/ 

Jumanne, 6 Novemba 2018

AFC: Miss Tanzania afunguka alivyotabiriwa na Mchungaji kushinda Miss World (VIA_AYO TV)

By

Tunayo story kutokea kwa Miss Tanzania, QueenElizabeth Mkune ambapo amesema alishawahi kutabiriwa kushinda taji hilo la Miss Tanzania pamoja na Taji la Miss World, ambapo mashindano yake yanatarajiwa kufanyika Sanya, China December 8,2018.
Katika exclusive interview na Ayo Tv, QueenElizabeth amesema utabiri wa kushinda Miss Tanzania ulitolewa na Mchungaji wa kanisa la Ufunuo, Nabii Paul Bendera na kwamba sasa amemtabiria tena atashinda taji la Miss World.
“Siri ya mafanikio yangu ni Mungu, kwa sababu siwezi kushinda kwa sababu ni mrembo kwani wasichana wote ni warembo, hivyo kushinda kwangu ni kibali kutoka kwa Mungu.Pia kilichonishawishi ni kutaka kuwa Miss World,”amesema.
Pia QueenElizabeth amesema kabla ya kuwa Miss Tanzania alikuwa tayari ni mtu wa dini licha ya kuwa watu wanamwambia kwamba urembo hauingiliani na suala la kidini hasa kwa kuokoka.


Source: ayo TV and ayo.com: http://millardayo.com/6wey3/

Jumatano, 24 Oktoba 2018

AFC: Irene Robert - Bongofleva wote waimbe Injili mziki wao haunisaidii | Gospel kupigwa Club poa tu

By

 
Msanii wa Muziki wa Injili Irene Robert ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Kishindo’amekaa katika Interview na AyoTV na millardayo.com ambapo amezungumzia wimbo wake wa Kishindo pamoja na mambo mengine kama utofauti wa nyimbo za Gospel na Bongofleva.
Irene Robert amesema ni furaha yake kuona waimbaji wa nyimbo za Bongofleva wakiimba nyimbo za Gospel ili kumtukuza Mungu nakusema sio kwamba wao wana-copy wanachofanya Bongofleva bali ni kuendana na wakati uliopo.
Irene Robert Hata wa Bongofleva walitakiwa wamuimbie Mungu, Mimi natamani sana waimbaji wote wa Bongofleva waimbe Injili ili kumtukuza”. 

  
Chanzo: AyoTV na millardayo.com

Ijumaa, 28 Septemba 2018

AFC: Wasifu - Khery Sameer Rajab (Mr Blue)

Image result for images of mr blue
Khery Sameer Rajab (amezaliwa tar. 14 Aprili 1987) ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue. Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue'. Ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.
Mr Blue alikuwa gumzo na wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na maujanja ya ala ya muziki wenyewe.
Image result for images of mr blue
Maisha ya awali
Mr Blue alizaliwa 14 Aprili mwaka 1987, ni mtoto wa tatu kati ya wanne kwa kuzaliwa katika familia ya mzee Sameer Alhaji Alhad Ally mwenye asili ya Ki-Sudan.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya Gerezani ambako alihitimu mwaka 1999, lakini hakuweza kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, ambako aliishia kidato cha pili mwaka 2004.
Alipoulizwa ni kitu gani kilichosababisha hadi kukatisha masomo ya sekondari, alisema: "Muziki ndio ulionifanya nikaacha shule, lakini bado nahitaji kusoma na baada ya muda kadhaa nategemea kujiendeleza kimasomo nje ya nchi." Japo baadae mwaka 2014 alikuja kufafanua changamoto zilizokuwa zikimkabili katika kipindi cha televisheni kiitwacho mkasi, kinachoongozwa na Salama Jabir, kikubwa alisema mahitaji ya kifedha yalikuwa makubwa na ulifika wakati alilazimika aidha kuchagua muziki au shule, kwa kuwa muziki ulikuwa ukitatua tatizo la kifedha, basi hakuwa na budi kuchagua muziki.
Akizungumzia hatua waliyochukua wazazi wake kutokana na kuacha kwake shule kwa sababu ya muziki, anasema hawakumgombeza kwani walijua ni ujana tu unamsumbua huku wakiamini itafikia wakati atatulia.
Image result for images of mr blue
Muziki
Mr Blue alianza kujihusisha na masuala ya muziki mwaka 1999, na kilicho sababisha ajiingize katika fani hiyo ni kaka zake waaliojulikana kwa majina ya The Boy Stain na Obrey, ambao nao walikuwa wakijihusisha na suala zima la muziki.
Lakini hakuanza kuimba moja kwa moja, bali alikuwa akifuatilia tu jinsi gani muziki unavyokua, na mwaka 2001 ndipo nilipojiingiza zaidi kwa kuanza kuimba katika sherehe mbalimbali za 'Macamp.
"Mwaka 2003 kuelekea 2004 ndipo alipotoka na wimbo wake wa 'Mr Blue' ambao ndiyo ulioanza kumapatia umaarufu.
Wakati akitamba na kibao chake hicho, lakini hakutaka mashabiki wamsahau mapema, hivyo aliamua kutoa kibao kingine kilichokwenda kwa jina la 'Mapozi', ambacho kilimtangaza na kupiga hatua kupitia nyimbo hizo.
Mr Blue ambaye albamu yake ya kwanza ilikwenda kwa jina la 'Mr Blue' na ya pili ni 'Yote Kheri'.
Pia anawashukuru mama yake mzazi Halima Rajab na baba yake Sameer Alhaj Alhad Ally kwa kumruhusu kujikita katika muziki. Pia aliwahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzake anayejulikana kama Naj anayeishi jijini London. uhusiano huo uliisha kitambo kidogo na sasa Mr. Blue ana mke.

Source: https://sw.wikipedia.org/wiki/Mr._Blue