Jokate Mwegelo | |
---|---|
Amezaliwa | Jokate Urban Mwegelo 20 Machi 1987 |
Utaifa Majina mengine | MTanzania Jojo Kidoti |
Mhitimu | Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam(Shahada ya Sayansi ya Siasa) |
Kazi yake | Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji, mwanasiasa |
Jokate Mwegelo ni mwigizaji wa filamu, mjasiriamali, mtangaziji, mwimbaji na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania. Kwenye mwezi Julai 2018 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
Jokate
vilevile alikuwa mtangazaji na mwimbaji halafu Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.
Mwaka
wa 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji filamu bora wa kike. Mwaka wa
2017, Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes
30 Under 30 kutoka Afrika.
Maisha ya awali na
elimu
Mwegelo alizaliwa tarehe 20 Machi 1987, huko mjini Washington, D.C, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.
Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alianza elimu ya msingi katika shule ya
Olympio Primary School na baadaye St. Anthony High School, halafu Loyola High School,
Dar es Salaam.
Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.
Miss Tanzania 2006
Alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Miss
Tanzania mwaka 2006. Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds
fashion na balozi wa gazeti la Citizen, baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.
Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006,
shindano ambalo alishinda, kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006, ambako pia alishinda.
kazi
Kuigiza
Mwaka wa 2007, alipata kucheza filamu yake ya kwanza
iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors, akiwa na Vincent Kigosi, Lisa Jensen, mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na
marehemu Adam Kuambiana.
Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With
True Love
Mwaka wa 2010, alionekana katika filamu ya Chumo, filamu
iliyoandaliwa na Media for
Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria. Filamu hii ilimwezesha kupata tuzo
ya Zanzibar
International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa 2011 na kuchaguliwa
kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards.
Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa TV maarufu
wa Siri Ya
Mtungi, uliokuwa unaandaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani,
mnamo 2013. Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa
"Ndekwa" katika filamu ya Mikono Salama, ambayo
ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar
International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.
Kampuni ya Kidoti
Muziki
Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa
na A.Y. katika
wimbo wa Kings and Queen, na Amani,
kutoka Kenya. Mwaaka
wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci, uliyoitwa 'Kaka na Dada. Mwaka wa 2015m, akadondosha wimbo wake
mwingine uliyoitwa Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.
Siasa
Jokate hakujulikana kujishughulisha na siasa hadi mwaka 2017
alipoteuliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha CCM(UVCCM)
kuongoza Idara ya Uahamasishaji na Chipukizi ya umoja huu akiwa kaimu katibu wa
idara hii. Yeye mwenyewe alitaja maarifa ya utoto wake alipohamasishwa na bibi
yake aliyekuwa mwasisi wa Umoja wa Walimu Tanzania katika Mkoa wa Rukwa kuona
ni muhimu kujitoa katika jamii na kuchukua nafasi za uongozi. Wakati ule magazeti yalileta taarifa
kuwa uteuzi wake ulipingwa na sehemu ya viongozi wa umoja huu.
Kwenye mwezi wa Machi 2018 aliondolewa katika nafasi hii kwa
azimio la kamati kuu ya UVCCM.
Mwisho wa mwezi wa Julai
2018 aliteuliwa na rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, uteuzi ambao ulileta cheche nyingi
katika uwanja wa mitandao nchini Tanzania. Wapo waliobeza uteuzi huo, wapo
waliosifia. Wengine waliweka picha zake za zamani
zilizokuwa hazina maadili ili kukebehi
uteuzi huo.
Filamu
- Movies
Mwaka | Filamu | Uhusika | Washiriki |
---|---|---|---|
2007 | Fake Pastors | Jackie | Vincent Kigosi, Adam Kuambiana, Lisa Jensen na Ahmed Ulotu |
2008 | From China With Love | Vincent Kigosi, Blandina Chagula, Suzan Lewis na Aileen Francisco | |
2011 | Chumo | Amina | Yusuph Mlela, Hussein Mkiety (Sharobaro) |
2014 | Mikono Salama | Ndekwa | Jacob Steven, Single Mtambalike na Irene Uwoya |
- Mfululizo wa TV
Mwaka | Mfululizo | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2013-2014 | Siri Ya Mtungi Msimu wa 2 | Mwanamitindo |
Diskografia
- 2013
Kaka Dada akiwa na Lucci
- 2015
Leo Leo akiwa Ice Prince
Awards and nominations
Year | Event | Prize | Recipient | Result |
---|---|---|---|---|
2008 | Ijumaa Sexiest Girl | Sexiest Girl | Herself | Won |
2011 | Zanzibar International Film Festival | Best Actress | Chumo | Won |
2012 | 2012 Nigeria Entertainment Awards | Pan African Actress Of The Year | Chumo | Nominated |
2013 | Swahili Fashion Week Awards | Female Stylish Personality Award | Herself | Won |
Under30 Youth Awards | Fashion Category | Herself | Won | |
2015 | Zanzibar International Film Festival | Best Actress Swahili Films | Mikono Salama | Won |
Swahili Fashion Week Awards | Baileys Female Stylish Personality | Herself | Won | |
2017 | Clouds Fm Malkia Wa Nguvu Awards | Business Innovation | Herself | Won |
Africa Youth Awards | Enterpreneur Of The Year | Herself | Nominated | |
Startup Of The Year | Kidoti Company | Nominated |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni