Khery Sameer Rajab (amezaliwa tar. 14 Aprili 1987) ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue.
Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki,
mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue'. Ambapo
baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.
Mr Blue alikuwa gumzo na wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu
zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi
na sauti aliyotumia pamoja na maujanja ya ala ya muziki wenyewe.
Maisha ya awali
Mr Blue
alizaliwa 14 Aprili mwaka 1987, ni mtoto wa tatu kati ya wanne kwa kuzaliwa
katika familia ya mzee Sameer Alhaji Alhad Ally mwenye asili ya Ki-Sudan.
Elimu yake ya msingi aliipata katika
shule ya Gerezani ambako alihitimu mwaka 1999, lakini hakuweza kumaliza elimu
ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, ambako aliishia kidato
cha pili mwaka 2004.
Alipoulizwa ni kitu gani
kilichosababisha hadi kukatisha masomo ya sekondari, alisema: "Muziki ndio
ulionifanya nikaacha shule, lakini bado nahitaji kusoma na baada ya muda kadhaa
nategemea kujiendeleza kimasomo nje ya nchi." Japo baadae mwaka 2014
alikuja kufafanua changamoto zilizokuwa zikimkabili katika kipindi cha
televisheni kiitwacho mkasi, kinachoongozwa na Salama Jabir, kikubwa alisema
mahitaji ya kifedha yalikuwa makubwa na ulifika wakati alilazimika aidha
kuchagua muziki au shule, kwa kuwa muziki ulikuwa ukitatua tatizo la kifedha,
basi hakuwa na budi kuchagua muziki.
Akizungumzia hatua waliyochukua
wazazi wake kutokana na kuacha kwake shule kwa sababu ya muziki, anasema
hawakumgombeza kwani walijua ni ujana tu unamsumbua huku wakiamini itafikia
wakati atatulia.
Muziki
Mr Blue alianza kujihusisha na
masuala ya muziki mwaka 1999, na kilicho sababisha ajiingize katika fani hiyo
ni kaka zake waaliojulikana kwa majina ya The Boy Stain na Obrey, ambao nao
walikuwa wakijihusisha na suala zima la muziki.
Lakini hakuanza kuimba moja kwa moja, bali alikuwa
akifuatilia tu jinsi gani muziki unavyokua, na mwaka 2001 ndipo nilipojiingiza
zaidi kwa kuanza kuimba katika sherehe mbalimbali za 'Macamp.
"Mwaka 2003 kuelekea 2004 ndipo alipotoka na wimbo
wake wa 'Mr Blue' ambao ndiyo ulioanza kumapatia umaarufu.
Wakati akitamba na kibao chake hicho, lakini hakutaka
mashabiki wamsahau mapema, hivyo aliamua kutoa kibao kingine kilichokwenda kwa
jina la 'Mapozi', ambacho kilimtangaza na kupiga hatua kupitia nyimbo hizo.
Mr Blue ambaye albamu yake ya kwanza ilikwenda kwa jina la
'Mr Blue' na ya pili ni 'Yote Kheri'.
Pia anawashukuru mama yake mzazi Halima Rajab na baba yake
Sameer Alhaj Alhad Ally kwa kumruhusu kujikita katika muziki. Pia aliwahi
kuwa na mahusiano na msanii mwenzake anayejulikana kama Naj anayeishi jijini
London. uhusiano huo uliisha kitambo kidogo na sasa Mr. Blue ana mke.