Jumamosi, 19 Mei 2018

AFC: Wasifu - Ramadhani Mtoro Ongala (Remmy Ongala)

.
Resultado de imagem para wasifu ya Remmy Ongala

Remmy Ongala (10 Februari 1947 - 12 Desemba 2010) alikuwa mwanamuziki nchini Tanzania mwenye asili ya Zaire. Alizaliwa na jina la kiraia la Ramadhani Mtoro Ongala katika jimbo la Kivu la Kongo ya Kibelgiji. Remmy alifahamika sana kwa uwezo wake wa kutungia nyimbo akiwa jukwaani. Mbali na zile anazotunga akiwa na wenziwe, lakini akiwa katika kumbi huwa anazifanyia manjonjo zaidi ya yale aliyotungia. Alikuwa mbunifu na kipenzi cha watu. Licha ya kuingia katika dini mbalimbali mwisho akaishia kuwa Mlokole hadi kifo chake.
Remmy Ongala pamoja na bendi yake ya Super Matimila, ni mashuhuri sana nchini Tanzania, na wamepiga muziki mara nyingi katika nchi za Ulaya na Marekani. Remmy Ongala kwa asili anatoka Zaire. Akiwa na umri wa miaka tisa mama yake alifariki, hivyo ikimbidi achukue jukumu la kutunza wadogo zake.
Akiwa na umri wa miaka 17, alikuwa muimbaji na mpiga ngoma katika bendi ya vijana ya Bantu Success. Hii haikuwa na maana kwa familia yake, hivyo Remmy ilimbidi atoke katika bendi. Miaka miwili baadaye, alijishughulisha tena na muziki. Alijiunga na vikundi mbalimbali vya bendi za muziki akiwa mpiga gitaa na baadhi yake zilikuwa Micky Jazz ya Zaire na Grand Mike Jazz ya huko Uganda. Mwaka 1978 alihamia Tanzania na kujiunga na bendi ya mjomba wake Ochestre Makassy ya jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1981 alijiunga na bendi ya Matimila, ikiwa na wanamuziki 18 na ikimilikiwa na mfanya biashara mmoja. Baadaye alianzisha bendi yake ya Super Matimila na kuendeleza mtindo wa kutumia magitaa 3, besi, ngoma na tarumbeta aina ya saksafoni. Remmy Ongala alipiga muziki wake kwa mtindo wa Soukous, katika maumbile mapya kabisa kwa kutumia asili na jadi ya kitanzania. Akiimba kwa kiswahili, ushairi wake mzuri una tunzi zinazohusu siasa na pia maisha ya mtu wa kawaida. Kwa ajili ya uimbaji na utunzi wake wa kuliwaza, Remmy anaitwa “Dokta” na ni mtu anayejulikana sana katika sehemu za Sinza ambazo ni jirani na anakoishi yeye na mkewe Mwingereza na watoto wao 5 na kasuku mmoja, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Albamu Alizotoa

·         1. Songs for the Poor Man (1989)
·         2. Mambo (1992)
·         3. Sema (1995)
·         4. The Kershaw Sessions (1995)

Viungo vya Nje:


Alhamisi, 17 Mei 2018

AFC: Wasifu - Khadija Omar Abdallah Kopa (Khadija Kopa)


"Siku moja nilikuwa nimekaa nikiiga wimbo. Akapita babu yangu aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akaniambia najua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuniandikia barua mwenyewe bila kunishauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba nijiunge nao".














Khadija Omar Abdallah Kopa (amezaliwa 1963 huko Zanzibar) ni mwimbaji wa muziki wa Taarabmtunzi wa nyimbo na mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa ushirikiano wake mkubwa na bendi ya TOT. Ameanza kuimba Taarab tangu 1990 na bendi ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa Culture Musical Club.
Maisha na kazi
Khadija Kopa alizaliwa mwaka 1963 kisiwani Zanzibar na ni mtoto wa kipekee katika familia ya Kopa. Ameolewa na ana watoto wanne na wajukuu wawili. Kazi ya sanaa alianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical Club. Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia mwanaharakati wa kisiasa nchini Tanzania. Khadija alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo, akisomea madrasa Zanzibar. Akiwa chuoni (madrasa) alikuwa msomaji mzuri wa qaswida, halafu vilevile alipokuwa Young Pioneer, alikuwa kwenye kikundi cha kwaya. Halkadhalika Shuleni alikuwa kwenye mambo ya ngoma, mambo ya utamaduni na kwaya. Shule yao ilikuwa bingwa kwa kwaya Zanzibar. Aliendelea hivyo hadi katika shule ya upili.
Siku moja alikuwa amekaa huku akiiga wimbo. Akapita babu yake aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akamsifia ya kwamba anajua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuandika barua kwa niaba yake bila ya kumshauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba ajiunge nao. Khadija pia amepata kushirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir, marehemu Leila Khatib na wanaume kama akina Abdul Misambano na Ali Star, waliporomosha nyimbo ambazo zilitamba miaka hiyo katika ulimwengu wa Taarab.

AFC: Wasifu - Naseeb Abdul Juma (DIAMOND PLATNUMZ)

Naseeb Abdul Juma (alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989) Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama DIAMOND PLATNUMZ. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote  na ikabidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi  yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao.. Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa "binadamu wabaya", Bofya hapa: https://www.youtube.com/watch?v=hSDilTuo2Gg.

Resultado de imagem para Diamond platnumz

Elimu
Mnamo mwaka 1995  alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo  Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani  (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi  iliyopo jijin Dar-es-salaam. Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano  diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy  baadhi ya na kukrem nyimbo za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya  nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti.
Resultado de imagem para Diamond platnumz

Sanaa ya muziki na utoto
Mara nyingi mama yake alikuwa akimnunulia kanda za album  za wasanii tofauti  waliokuwa wakihit kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za  wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati  mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya tallent show  ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa  familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya  kumuhimiza kimasomo. Kiukweli hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu saana, maana mama Diamond hakuwa hana source ya kumuingizia kipato, hivyo  ilibidi atumie kias kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili  alivyopewa na Mama yake yaani bibi yake diamond na vibiashara vyake  vidogovidogo vya mikopo kwa kumsomeshea na kumlea diamond, hakika hali  yao ya Kimaisha ilikuwa ni ngumu sana, hivyo iliwaradhimu wote kuhamia  katika chumba cha bibi huyo ili kupangisha vyumba vile viwili alivyopewa mama diamond…


Resultado de imagem para Diamond platnumz

Ugumu
Baada ya kuhitimu shule ya Msingi mwaka 2002 na kutaka  kuanza masomo ya Secondary mwaka 2003  mama yake alimwambia aachane na Muziki kabisa na azingatie na Masomo ili aweze kupata elimu itayomsaidia hata kwa muziki wake baadae kwa maana asingeweza kushika vitu viwili  kwa pamoja muda huo. Akiwa secondary diamond aliendelea kufanya muziki  kisirisiri bila mama yake kujua na kufikia mwaka 2004 taratibu akaanza  kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe. Baada ya kuhitimu elimu yake ya Secondary mwaka 2006 mwaka 2007 alijikita rasmi katkia sughuri za  muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.

kiukweli haikuwa ni safari  rahisi kama alivyotegemea hadi kupelekea time kuanza kutafuta vibarua  toafauti tofauti ili mradi aweze kupata riziki na kuepuka hali ya  kushinda nyumbani, ikiwemo kuuza mitumba, petrol station, kupiga picha,  kupigisha simu, kazi za viwandani hata wakati mwingine kuingia kwenye  makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia  studio kurecord lakini bila kufanikiwa, kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana hadi ikamradhimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi aivae na kumdanganya kuwa ameipoteza na ndipo hapo alipofanikiwa  kuingia studio kurecord nyimbo ya kwanza iitwayo toka mwanzo..
kutokana na kutokuwa na mazoea ya kurecord hakuweza kutengeneza nyimbo ambayo ni  hit lakini wimbo ule ulianza kumpa conections tofauti tofauti maana wengi walishangazwa jinsi alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza  kutengeneza wimbo kama mtu ambae ni mzoefu, hivyo iliwafanya kuamini  kuwa akipata nafasi ya kurecord mara kadhaa angeweza kufanya kitu  kikubwa.. wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo mapene ambae  alijitolea kumsimamia, na kweli wakaanza kurecord album lakini bahati mbaya wakiwa katikati ya kurekodi album hiyo anayemsaidia alipata  matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia hivyo ilimbidi  Diamond aanze tena upya kuzunguka katika studio tofauti kuomba  kusigniwa kwenye record label lakini kote hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado kuimba hajui na kuto kutaka kumsikiliza kabisa…
kiukweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambae alikuwa nae alimuacha kwakua alikuwa ameshachoshwa na ndoto hewa ambazo  alikuwa akiziota kila siku diamond kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki na kuwa mwanamuziki mkubwa na wao kuish maisha mazuri, kitu ambacho kilimchanganya na kumuumiza sana diamond hususan kwa kauli aliyomuambia ya “skiza Diamond mi kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana maslahi kwangu” kutwa ilikuwa ikimpitia kwenye kichwa na kujiona kama mwenye mikosi.


Resultado de imagem para Diamond platnumz

Mafanikio

Mwaka 2009,  Diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter  maarufu  kama Papaa Misifa ambae alikubali kumsaidia kimuziki na Kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la “Nenda kamwambie”, wimbo  ambao Diamond aliimba  kwa uchungu  huku akimuimbia mpenzi wake huyo aliyemuacha (Sarah Sadiki) kuelezea kiasi  gani  aliumia kwa yeye kumuacha kwake, na hapo ndipo taratiibu nyota yake ikaanza kung’aa na wimbo huo kukua siku hadi siku.Maisha yake yakabadilika  na Diamond kuweza  kununua gari  aina ya Toyota Celica.
Tarehe  14/02/2010 Diamond aliachia  album yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 10 ambazo ni kamwambie  , Mbagala  , Nitarejea  , Nalia na mengi , Binadamu  , Nakupa  , Usisahau  , Uko tayari  , Wakunesanesa  , Toka mwanzo  na Jisachi. Mnamo tarehe 04 mwezi wa  4 mwaka 2010 , Diamond aliandika record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards kwa pamoja ambazo ni: Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa Mwaka (KAMWAMBIE) na  Wimbo bora wa R&B(KAMWAMBIE), tunzo ambazo zilimfanya achaguliwe  kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania.

Baada ya kuachia wimbo wake wa  pili  unaoitwa Mbagala,  Diamond alichaguliwa na Rais wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete kuwa  Entertainer katika tour nzima ya Kampeni yake.  Tarehe 02 mwezi wa 10 mwaka 2010 alipata  tour ya kwanza kwenda England mjini LONDON,MILTON KEYNES, na COVENTRY.  Baada ya  kuachia  wimbo wake wa tatu mwaka 2011  , Diamond alishinda tuzo ya Nzumari  Award nchini Kenya akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka  Tanzania.  Diamond alirelease nyimbo yake ya nne na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha hadi watu  kushindwa kuingia na hata wengine kuzimia baada kutokupata hewa ya kutosha kutokna na wingi ujaaji huo.

Mwaka mpya wa 2012, tarehe 1 mwezi wa kwanza mwaka 2012 , Diamond Platnumz aliachia album yake ya pili  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya 1200,000 ulbum Copies. Mwanzoni mwa mwaka 2012 Diamond aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya Corparate iliyoitwa ” Diamons are forever” iliyofanyika Mlimani City  kwa kiinglio  cha shilingi elf hamsini 50,000  za kitanzania akiwa pekeake na show kuwa sold ot kwa zaidi ya ticket 1,500.

Mnamo mwezi wa tano mwaka 2012 , Diamond Platnumz  aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu 10’000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive  huku akishuka na Helicopter kwenye Stage. Mwaka huohuo  Diamond alifanya ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland, Sweden ,  Greece na kumalizia ziara yake ya arabuni nchini Masqat  Oman.

Mwishoni mwa mwaka 2012 ulikua mzuri kwa Diamond Platnumz kwani aliweza kuachia nyimbo mbili kwa mpigo za “Nataka kulewa ” na “Kesho ” zilizoambata na video zake.Mwezi wa kumi na mbili mwaka  2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi kwenye Show toka Tanzania.


Mwanzoni mwa mwaka 2013 , Diamond  Platnumz alichaguliwa na Cocacola kuwa Brand Ambassador wa Kinywaji Cha Cocacola, na  kufuatiwa na ziara yake ya East Africa na ikiwemo Burundi  , Congo na Kenya n.k. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza East Africa kuweza.
kupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000… mnamo  June 2013 Diamond alishinda tuzo mbili  za Tanzania Kili Music  Award akiwa kama   Msanii bora wa kiume Bongoflavour na Msanii bora  wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania.

Mwezi wa saba mwaka 2013 , Diamond  alirelease next single yake iliyokwenda kwa jina la Number One ambayo  aliifanyia Video Capetown South Africa Chini ya kampuni ya Ogopa  Videos  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila kiingilio katika Hotel ya SERENA na kuwaalika CEO’s  ,  mameneja  na  viongozi toka sehemu tofauti tofauti. katika launching hiyo akamzawadia Gari moja ya Malegend wakubwa katika mziki wa Tanzania , Marehemu  Mwidini Gurumo.

Resultado de imagem para Diamond platnumz


Kimataifa

mwezi 10 mwaka 2013  , Diamond aliifanya Collabo na msanii toka Nigeria  Davido ya ngoma ya Number one kama Remix na kisha kwenda nchini Nigeria  kwajili ya kusomea Markert ya West Africa na kushoot video ya wimbo huo  ulio shootiwa na Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director  Clarence Peter. Nyimbo hii ilimtambulisha Diamond Platnumz nchini Nigeria na barani Africa kiujumla na kumuwezesha kupata nominations mbalimbali kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo , MTV MAMA awards ambayo aliperform nyimbo hii live na Davido, BET Awards na tuzo zinazotegemea kufanyika za AFRIMAMA , MTV Europe , Channel O awards na awards nyingine kutoka nchi mbalimbali.
Tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 2014 , wakati Diamond akisherekea Birthday ya mama yake alimzawadia mama yake gari pamoja na kuachia video mbili za mdogomdogo aliyoifanyia nchini Uingereza na BumBum aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliifanyia Afrika Kusini. Video hizi  kwa pamoja zilimgarimu Diamond dola 78,000 za kimarekani . Hivi Sasa nyimbo hizi ndio habari ya mjini na ni kitu kisichofikisha kwamba nyimbo hizi zitaendelea kumbeba Diamond hadi mwaka 2014 unaisha.
Huyu ndio Diamond Platnumz, mtoto wa Tandale aliyoweza kutumia kipaji chake cha kuimba vizuri, aliyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ,maisha yake ni fundisho kwa vijana kibao mjini wanaohangaika kutoka kimaisha. Familia ya Vibe Tanzania inamtakia maisha marefu wakati huu anaposherekea kutimiza miaka 26 ya maisha yake iliyousisha uchungu , mahangaiko,tabu,kutafuta na baadae kumzawadia furaha pale anapoona mafanikio yanamjia.....



WatsUp TV Africa Video za Tuzo za Muziki
YearNominee/workAwardResultRef
2016KidogoAfrican Video of the YearWon
Best African Combo VideoWon
Best African PerformanceNominated
Best African Male VideoWon
Best East African VideoNominated

Channel O Music Video Awards

YearNominee/workAwardResult
2014"Number One"Most Gifted NewcomerWon
Most Gifted EastWon
Most Gifted Afro PopWon
Most Gifted Video of the YearNominated

HiPipo Music Awards

YearNominee/workAwardResult
2015"Number One"East Africa SuperhitWon

Top Ten Tube Music Awards

YearNominee/workAwardResult
2014"Diamond Platnumz"Best Artist East AfricaWon

The Headies

YearNominee/workAwardResult
2014HimselfAfrican Artiste of the YearNominated

The Future Africa Awards

YearNominee/workAwardResult
2014HimselfPrize in EntertainmentWon

Nzumari Awards

YearNominee/workAwardResult
2012"Diamond"Best Male Artist – TanzaniaWon

MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA

YearNominee/workAwardResult
2014HimselfBest African ActNominated
2015himselfBest African ActWon
2015himselfworldwide act (Africa/India)Won

MTV Africa Music Awards

YearNominee/workAwardResult
2010DiamondBest New ArtistNominated
2014DiamondBest MaleNominated
Diamond (featuring Davido)Best CollaborationNominated
2015DiamondBest MaleNominated
Best Collaboration (BumBum Ft Iyanya)Nominated
Best Live ActWon
2016DiamondBest Male ArtistNominated
Artist of the yearNominated

BET Awards

YearNominee/workAwardResult
2014DiamondBest International Act: AfricaNominated
2016DiamondBest International Act: AfricaNominated

African Muzik Magazine Awards

YearNominee/workAwardResult
2014HimselfBest Male East AfricaWon
Artist of the YearNominated
"Number One"Best Video of the YearNominated
"Number One Remix"Best CollaboNominated
Song of the YearNominated
2015himselfBest Male Artist East AfricaWon
NanaVideo of the yearWon
HimselfArtist Of The YearWon
Alive with BracketAfrimma Best Insipirational SongWon
Nana Ft Flavour N'abaniaBest CollaborationNominated
NanaBest Dance VideoNominated
Nitampata WapiSong Of The YearNominated

Tanzania Music Awards

YearNominee/workAwardResult
2010DiamondBest Upcoming ArtistWon
"Kamwambie"Best SongWon
Best R&B SongWon
2011DiamondBest Male SingerNominated
Best Male ArtistNominated
Best Afro Pop Song "Mbagala"Nominated
Best Video "Mbagala"Nominated
2012DiamondBest Male ArtistWon
Best Song WriterWon
Best Male SingerNominated
"Moyo Wangu"Best Music VideoWon
Best Song of the yearNominated
Afro Pop Song of the YearNominated
2013DiamondBest Male ArtistWon
Best Male SingerWon
2014DiamondBest Male ArtistWon
Best Male WriterWon
Best Male Entertainer of the YearWon
"Muziki Gani" (Nay Wamitego featuring Diamond)Best Collaboration SongWon
"Number One"Best Afro Pop SongWon
Best Music VideoWon
Song of the yearWon
2015DiamondBest Male ArtistNominated
Best Male PerformerNominated
Songwriter of the YearNominated
Mdogo MdogoAfro Pop Song of the YearNominated
Video of the YearWon
Nitampata WapiBest Zouk/Rhumba SongWon
KerewaBest CollaborationNominated

Tanzania People's Choice Awards

YearNominee/workAwardResult
2014My Number OneFavourite Male VideoWon
2015DiamondFavourite Male ArtistNominated
Marejeleo
1. http://kikoti.blogspot.com/2015/10/fahamu-historia-ya-diamond-na-ali-kiba.html
2. https://en.wikipedia.org/wiki/Diamond_Platnumz
3.https://web.archive.org/web/20140607005318/http://www.diamondtz.com/artist/diamond-platnumz-english-biography/
4.https://channelo.dstv.com/2012/05/stargame-gig-guide-2/
5.http://www.bongo5.com/mastaa-20-wa-burudanimichezo-na-urembo-tanzania-wenye-ushawishi-mkubwa-zaidi-04-2013/
6. https://www.youtube.com/watch?v=2DlUeI8T6FY
7.https://www.youtube.com/watch?v=9gNyERFAm14&t=30m15s
8. https://www.youtube.com/watch?v=QkZdDn2U6iI
9.https://www.bellanaija.com/2016/10/yemi-alade-wizkid-diamond-platnumz-cassper-nyovest-others-nominated-for-watsup-tv-africa-music-video-awards-set-to-hold-this-december/
10.https://mg.co.za/article/2014-09-05-channel-o-africa-announces-music-video-awards-nominees
11.http://www.premiumtimesng.com/entertainment/music/172103-tanzanian-south-african-floor-nigerias-davido-channel-o-music-awards.html 
12.http://www.premiumtimesng.com/entertainment/168016-davido-nominated-for-mtv-europe-awards.html
13.https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/entertainment/artikel.php?ID=318709
14.https://www.bellanaija.com/2014/06/see-the-nominees-for-the-african-muzik-magazine-awards-afrimma-2014/
15.http://www.premiumtimesng.com/entertainment/165529-yaya-toure-ice-prince-davido-shortlisted-for-2014-future-africa-awards.html#sthash.lRcowZZX.dpbs
16.http://www.pulse.com.gh/entertainment/music/wamva-2016-bisa-kdei-shatta-wale-sarkodie-wizkid-flavour-others-nominated-id5557711.html
17.https://www.youtube.com/user/TheDiamondplatnumz
18.https://www.facebook.com/DiamondPlatnumz255/
19.https://itunes.apple.com/us/artist/diamond-platnumz/id721552376
20. https://www.bbc.co.uk/music/artists/a4dd4cc7-576d-4126-9780-75a48741234e
21.https://www.instagram.com/diamondplatnumz/
22.https://twitter.com/diamondplatnumz
23.http://www.djmwanga.com/2017/07/diamond-platnumz-eneka.html
24.https://music.howwe.biz/DiamondPlatnumz

25.http://www.news24.com/Drum/Archive/see-one-on-one-with-tanzanian-superstar-diamond-platnumz-20170728