"Siku moja nilikuwa nimekaa nikiiga wimbo. Akapita babu yangu
aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akaniambia najua
kuimba. Basi akachukua hatua ya kuniandikia barua mwenyewe bila kunishauri,
akaipeleka Culture Musical Club kuomba nijiunge nao".
Khadija Omar Abdallah Kopa (amezaliwa 1963 huko Zanzibar) ni mwimbaji wa muziki wa Taarab, mtunzi wa nyimbo na mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa ushirikiano wake mkubwa na bendi ya TOT. Ameanza kuimba Taarab tangu 1990 na bendi
ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa Culture Musical Club.
Maisha
na kazi
Khadija Kopa alizaliwa mwaka 1963 kisiwani Zanzibar na ni mtoto
wa kipekee katika familia ya Kopa. Ameolewa na ana watoto wanne na wajukuu
wawili. Kazi ya sanaa alianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical
Club. Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia
mwanaharakati wa kisiasa nchini Tanzania.
Khadija alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo, akisomea madrasa Zanzibar.
Akiwa chuoni (madrasa) alikuwa msomaji mzuri wa qaswida, halafu vilevile alipokuwa Young
Pioneer, alikuwa kwenye kikundi cha kwaya. Halkadhalika Shuleni alikuwa kwenye
mambo ya ngoma, mambo ya utamaduni na kwaya. Shule yao ilikuwa bingwa kwa kwaya
Zanzibar. Aliendelea hivyo hadi katika shule ya upili.
Siku moja alikuwa amekaa huku akiiga wimbo. Akapita babu yake
aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akamsifia ya kwamba
anajua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuandika barua kwa niaba yake bila ya
kumshauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba ajiunge nao. Khadija pia
amepata kushirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir,
marehemu Leila Khatib na wanaume kama
akina Abdul Misambano na Ali Star, waliporomosha nyimbo ambazo
zilitamba miaka hiyo katika ulimwengu wa Taarab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni